Monday, December 3, 2012

FOMU YA USAJILI YA WANAWAKE MASHUJAA TANZANIA



WANAWAKE MASHUJAA TANZANIA
P.O. Box 1873, Arusha – Tanzania. Tel. +255 682 622 626 / +255 766 445 733
 

FOMU YA USAJILI – Taasisi ya  Wanawake Mashujaa Tanzania

“Kama ndio - Karibu tuungane pamoja”

TAFADHALI JAZA FOMU HII KUWA UMEKUBALIANA:
JINA: ……………………………………….
SIMU: ………………………………............
ANWANI: …………………………………
BARUA PEPE: …………………………….
UMRI: …………………………..................
KAZI: ……………………………...............
JINSIA: ......................................................
MIAKA YA NDOA/MAHUSIANO: …………………………
IDADI YA WATOTO: …………………………………………

1.         Ni  mada gani utapenda  tuzungumzie/jadili  zaidi  (Orodhesha kwa           mpangilio)
            (a)       ……………………………………………………………………………………….
            (b)       ……………………………………………………………………………………….
            (c)       ……………………………………………………………………………………….

2.         Mara ulipopata taarifa ya Taasisi hii, Je? umefanya uamuzi wa  yafuatayo,     weka  alama ya   √   kwa yale ambayo ni sahihi:-

            (a)       …………….Uliamua kubadili tabia na kuwa shujaa mwaminifu?
            (b)       …………….Uliwaza kuwa ipo siku utakuwa Kiongozi wa jamii  yako?
            (c)       …………….Ulijua wewe ni wa thamani na Mwenzi/Mume                                                              uliye naye ni zawadi kutoka kwa Mungu?
            (d)       ……………Uliwaza kuwa ndoa uliyo nayo ni ya kuitunza sana na                    umepewa jukumu kubwa sana la kulea mume/mke na watoto wako vizuri?

3.         Utapendelea tuwe na Waalimu tofauti tofauti ili kujifunza mambo mazuri kuhusu malezi bora ya ndoa na watoto wetu? Kama ndiyo (Orodhesha  mambo matatu ambayo utapenda kujifunza)
            (a)       ……………………………………………………………………………………….
            (b)       ……………………………………………………………………………………….
            (c)       ……………………………………………………………………………………….

4.         Utapenda mada zingine zihusishwe? Kama ndiyo ni mada zipi? (Orodhesha        kwa mpangilio)
            (a)       ……………………………………………………………………………………….
            (b)       ……………………………………………………………………………………….
            (c)       ……………………………………………………………………………………….
            (d)       ……………………………………………………………………………………….

5.         Unalinganisha vipi mguso mzima wa Taasisi hii? Sehemu ambayo ni sahihi        tafadhali weka alama ya  √
            (a)       ………………………….Nzuri kupindukia
            (b)       ………………………….Nzuri sana
            (c)       ………………………….Nzuri
            (d)       ………………………….Wastani
            (e)       ………………………….Siyo mbaya sana
            (f)        ………………………….Ni mbaya

6.         Elezea ni nini uliona kabla ya kuanza mahusiano na baada ya kuanza       mahusiano hadi sasa.

            …………………………………………………………………………………………………
            …………………………………………………………………………………………………
            …………………………………………………………………………………………………
            …………………………………………………………………………………………………
            …………………………………………………………………………………………………
            …………………………………………………………………………………………………
 …………………………………………………………………………………………………
......................................................................................................................................................
        
  N:B Taarifa hizi zitatusaidia katika kufahamiana na kujua ni jinsi gani tunaweza kusaidiana wenyewe na jinsi ya kuweza kusaidia wengine ambao tunalengo la kuwafikia.
           
           
           
           






Imetayarishwa na:

Diana Didas Shirima 
(Community Development Officer)
Founder- WANAWAKE MASHUJAA TANZANIA

SEHEMU YA TATU NA YA MWISHO KWA MWAKA 2012, MADA ILIYO PANA NA INAYOSHIKILIA MAISHA YA WAPENDANAO ILIKUWA, NDOA,NDOA UNAYOILILIA UNAWEZA KUITUMIKIA?



Ndugu zangu wapendwa, napenda sana kutumia wakati huu kumshukuru Mungu aliyeniwezesha katika safari nzima ya mwaka 2012 nikiwa kama mwanaharakati mchanga katika gurudumu hili la Familia, Malezi na Mapenzi.

Ki ukweli hakuna kazi rahisi hapa duniani, kila jambo unalolifanya linachangamoto zake na mara zote nimejifunza kuvumilia na kusimama katika maono niliyonayo hadi kieleweke.

Unaweza ukasema kuwa wanaharakati wengi wanajiingiza katika uharakati kwa manufaa yao wenyewe, lakini mimi kama mimi ninapenda kusema kwamba uanaharakati nilianza tangu nikiwa mtoto mdogo, nakumbuka nikiwa darasa la pili Jijini Arusha, ndoto yangu ilikuwa niwe mama bora kwa familia yangu, mke mwema, na mwanamke shujaa kwa jamii inayonizunguka, namshukuru sana Mungu kwa asilimia 98%  nimefanikiwa kufikia malengo yangu.

Mara nyingine nimekutana na vikwazo mbalimbali hasa katika hatua za ukuaji, kama kijana wa kike nilipitia mengi sana, mengine kwa kujua na mengine kwa kutokujua lakini yote ya yote niliyaita mapito hayo kama DARASA kwangu ili leo niwe msaidizi wa kuwafungua wengine wanaopita katika maeneo niliyopita kwa ujasiri.

Unajua maana ya UJASIRI?  Ngoja leo nikudokeze japo kidogo, ujasiri maana yake ni kuvuka katika eneo gumu na kuendelea kuwa na uso wenye tabasamu la kudumu huku ukinyooshewa vidole na jamii husika. Unapojifunza kujikubali, ukatubu, ukabadilika na kusonga mbele tayari wewe ni SHUJAA. Ndio maana leo hii mimi nimesahau yote niliyoyatenda katika ujana wangu, nikajitambua na sasa nipo vizuri kusaidia jamii inayonizunguka iweze kutambua wajibu wao katika maisha ya kila siku.

Katika kai hii namshukuru Mungu nimekamilisha mwaka mmoja tangu niianze rasmi, niliianza kama kujitolea, baadae nikatoa fomu za kujiunga na chama ambazo bado zipo na zinauzwa kwa Tsh: 5,000/=  natumai kutokana na gharama za uendeshaji kuwa mgumu kila mwanachama mpya wa 2013 atakayependa kujiunga na chama atapaswa kuchangia Tsh. 10,000/=  ili tuweze kufikia malengo ya chama chetu ifikapo mwaka 2015.

Naamini jamii ya Tanzania inakilio kikubwa sana kuhusiana na swala hili la mahusiano, ndoa na maisha ndani ya ndoa. Lakini mbona wahusika tumekaa kimya? mbona kila kitu kipo wazi na tunaona jinsi ambavyo hali imekuwa mbaya katika maisha ya mahusiano alafu hatustuki, tunaona sawa tu! Hebu angalia waliopo nyuma yako, angalia kizazi kinachokuja hapo nyuma kutakuwa na NDOA kweli?

Sasa ndugu zangu naomba tusijisahau katika hili, tunahitaji mchango wenu ili kufikia malengo ya kuwasaidia wote waliopo katika mahusiano na walioingia katika taasisi ya ndoa ili wajitambue na kukaa katika mstari ulionyooka. Wewe na mimi tunaweza kuibadilisha mitazamo hasi kuwa chanya kuhusu mahusiano mema katika mapenzi na maisha ndani ya ndoa.

Naamini kabisa malengo yangu yatatimia katika swala hili la uanaharakati wa maswala ya familia, malezi na mahusiano ya kimapenzi, ili ifikapo 2015 tuwe tumeifikia Tanzania nzima kwa kutoa mafundisho na kusaidiana kuhusu saikolojia ya mapenzi na malezi ya watoto.

Nna mengi ya kuzungumza, lakini naomba nisikuchoshe, endapo utapenda kuwasiliana na mimi kwa ajili ya kujiunga na chama hiki, kufadhili chochote basi usisite kuwasiliana na mimi kwa namba zifuatazo:

DIANA DIDAS SHIRIMA
FOUNDER - WANAWAKE MASHUJAA TANZANIA
+255 766 44 57 33 / 682 622 626
didasdiana@gmail.com
www.wanawakemashujaatanzania.blogspot.com

MUNGU WA MBINGU NA NCHI AKUBARIKI SANA KWA KUJITOA KWA AJILI YA JAMII, MKE, MUME, NA WATOTO WAKO AMBAO WANAKUZUNGUKA! 
PAMOJA TUNAWEZA, KUBWA NI KUJIAMINI TU!

Wednesday, November 28, 2012

SEHEMU YA PILI YA MADA KUHUSU NDOA, NA MAISHA YA NDOA!

Natumai hujambo kabisa mpendwa wangu unaefuatilia makala zangu za NDOA, NDOA, UILILIAYO UNAWEZA KUITUMIKIA?  Ni swali ambalo limekuwa likiwaumiza watu wengi walio katika mahusiano na wengi zaidi ambao wanatamani kuingia katika mahusiano, leo tuangalie baadhi ya vitu ambavyo wengi wetu tumekuwa tukihisi tutavikuta katika mahusiano ya kimapenzi na endapo tukivikosa basi mahusiano huwa katika usawa wa kuvunjika au kuwa na migogoro isiyo kwisha.

UBINAFSI

 Huu nimeutafsiri kama kigezo cha kila aliepo katika mahusiano ya kimapenzi kuwa nacho kwa kusudi eidha zuri au baya, nasema hivi kwa sababu wote wawili tunavoingia au kutamani kuingia katika mahusiano huwa tunalenga kupokea vitendo vya mapenzi zaidi kutoka upande wa pili (mpenzi) huuangalii kama na wewe unahusika asilimia zile zile uoneshe kumpenda mwenzako, sasa kasheshe linakuja pale ambapo mwenzio anahitaji kujipendelea zaidi yeye apendwe, ni kwanini unataka upendwe wewe zaidi? Huyo akupendaye atapendwa na nani? wakati mwingine tumekuwa tukilaumu zaidi upande mmoja bila kugundua huo ni UBINAFSI, unakusumbua, jiachie alafu fanya zaidi ya vile unavyotamani ufanyiwe na mpenzi wako kisha utaona mabadiliko au siyo? Acha kulalamika na tafuta suluhu kwa amani!

TAMAA

Tamaa imechukua nafasi kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi kwani kila mmoja anatamani kutendewa vizuri sana na mpenzi wake katika mambo mengi sana, hivyo basi unapokuwa nje ya mahusiano ya kimapenzi huwa unatamani kufanya mambo mengi mazuri kwa mwenzio na mpenzi wako anakuwa anajiandaa kupokea zaidi kutoka kwako, gafla unapoingia katika mahusiano kila kitu kinabadilika kiasi kwamba hadi zile ahadi na mapenzi uliyoahidiwa hayaonekani, unadhani nini kitafuata? Kila mmoja huonesha ubabe wake halisi na kujitoa taratibu katika uhusiano bila upande mmoja kuelewa kinachoendelea. Umeshafahamu ni kwa nini mpenzi wako ana tabia aliyonayo sasa hivi? Angalia muenendo mzima wa tabia zake jinsi alivyobadilika kisha chukuwa hatua ya kujirekebisha wewe kwanza alafu ndo mkae pamoja kurekebishana!

Natamani kuendelea, lakini mda hauniruhusu kwa sasa, tuendelee kuwa pamoja wakati mwingine!
Ndo kwanza kumekucha, usichoke kusoma makala haya na upende kubadilika rafiki yangu na ujitahidi kusaidia wengine wabadilike.

Nakupenda na natamani ubadilike ili tuibadilishe jamiii yetu!

Imeandaliwa na,
Diana D. Shirima
Founder - Wanawake Mashujaa Tanzania

Sunday, November 25, 2012

NDOA, NDOA, NDOA, UNAYOILILIA JE UPO TAYARI KUITUMIKIA?





Habari ya leo mpendwa wangu, napenda kusaidiana na wewe katika mada yetu ya leo kama inavyojieleza katika kichwa cha habari hapo juu.

Mimi na wadau wenzangu wa maswala ya familia na maadili tumekuwa tukijiuliza maswali mengi kuhusu NDOA na MAISHA YA NDANI YA NDOA, na kung'amua yafuatayo ambayo kwa upande mmoja au mwingine yanaweza kukusaidia katika maamuzi ya kujiandaa kuingia katika taasisi hii kabla hujavamia au kujikuta unajuta baada ya muda mfupi sana.

Ni muda mrefu sana tumeshuhudia wanawake wengi sana wakifunga kwa maombi na wengine wakienda kwa waganga wa jadi kusafisha nyota ili waweze kupata waume wa kuwaoa/ na wanaume pia wamekuwa wakisumbuliwa sana na hali hii hatimaye nawao wanahangaika kutafuta wakuweza kuoa na kuishi nae milele. Siyo mbaya kabisa kufikia uamuzi/ maamuzi hayo, lakini swali ni kwamba Je? umejiandaa vipi kuishi maisha ya ndani na huyo unaemtaka? au unayemuombea kila siku? Muda mwingi wengi wetu tumekuwa tukitamani kitu ambacho kwa nje huwa hatukielewi haraka, badala yake tumekuwa tukiamua kirahisi rahisi tu ili kutimiza ndoto zetu za kuwa mume/mke wa mtu bila kuangalia ni jinsi gani tunaenda kuishi huko ndani, wengine huwa mnasema, " haina shida, nkifika ndani, nitajitahidi kumrekebisha, na hiyo tabia ya ulevi kupindukia ataiacha." unahisi ni kazi rahisi kumbadilisha mtu mzima ambaye ukoo wake mzima ni yeye tu ndo anakunywa bia laini, na walio salia wote wanywaji wa GRANTS na WISKY? unahisi wazazi wake walivokuwa wanamsisitiza apunguze ulevi walikuwa wajinga? Leo wewe ambaye hujajipanga chochote zaidi ya kelele zako na mdomo wako mchafu, ndo utambadilisha? Hebu jiulize swali hili, wazazi na ndugu zake tangu anakuwa walizoea kumuona akija nyumbani saa sita usiku, huwa hawasemi kitu, wewe leo na sheria zako mpya unamfokea tu na kumlazimisha arudi saa mbili, inawezekana kweli kirahisi?

Mwingine yeye hayawahi kuona baba na mama yake wakikaa mezani kula pamoja hata siku moja, sana sana wageni wakija ndo wanaweza kukaa pamoja tena wale wageni wa muhimu sana, leo wewe umetoka katika familia yenu, kila siku jioni ni lazima wote muwe mezani (dinning) kwa chakula, na huwa mna mazoea ya kusali kabla ya kula na pia mkimaliza kula mnasali kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya siku hiyo kisha kila mmoja anatawanyika kwenda kulala, sasa mume wako au mkeo hana tabia hiyo na kwake ni kero kubwa pale unapomlazimisha, unafanyaje kukabiliana na swala hilo? Kila unapojitahidi kumuhamasisha aje mezani yeye haoni umuhimu, amekazana kuangalia TV, au kakazana kuchat na friends zake wa facebook and tweeter, inakuwaje? Duuuu! kama nakuona vile unavyonuna usiku mzima, unajijutia lakini ufanyaje? tayari ushaingia kwenye ndoa ndugu yangu!

Ni mambo mengi sana yapo katika hii mada, ila kwa leo tunaishia hapo natamani sana kuendelea ila mda hautoshi na mie sitaki usome kama gazeti kwani kujifunza ni kidogo kidogo, na umuhimu ni kufunguka ulipojifunga au siyo ndugu yangu? Usijali tupo pamoja na tutafika tu au siyo jamaniiii?

Hadi wakati mwingine, usikose kufuatilia makala nyingine inayoendeleza habari zaidi kuhusu NDOA, NA MAISHA NDANI YA NDOA!

Monday, October 29, 2012

TIBA KWA WANAUME IMEKUJA, SOMA HAPA UPATE ELIMU JUU YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UPATE MSAADA WA KISAIKOLOJIA.



 Tatizo la wanaume wengi la kukosa nguvu za kiume sasa limepata ufumbuzi wa hali ya juu kutoka kwa watafiti mbalimbali ambao hawalali mchana na usiku wakihangaika kupata ufumbuzi huu, na hizi ndio habari mpya walizonazo kwako wewe unaesumbuliwa na tatizo hili, karibu sana upate somo hapa!

Tafiti mbalimbali duniani zinabainisha kunaongezeko kubwa la watu wanaosumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume,  (ED au Erectile dysfunction).

Kulingana na taarifa za shirika liitwalo the National Ambulatory Medical Care Survey (NAMCS), nchini Marekani kati ya wanaume 1,000, watu 22 husumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume/kijinsia hasa wale wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea juu.

Aidha kutokana na kukithiri kwa tatizo hilo, NAMCS inasema zaidi ya watu 2.6 milioni wanatumia dawa za kuongeza nguvu za kiume. Hali ni mbaya pia nchini, hii ndio sababu kuna matangazo mengi ya waganga wa jadi wenye kutibu nguvu za kijinsia, kiasi kwamba inakuwa vigumu kufahamu yupi mkweli yupi mwongo.

Utafiti pia unaonyesha kuwa asilimia 5 ya wanaume wenye umri wa 31- 40 na kuendelea wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo, aidha kati ya asilimia 15 na 25 na wanaume wenye umri wa miaka 65 wanakabiliwa na tatizo hili.

Nimewahi kupitia  vitabu kadhaa, kwa mfano kile kiitwacho ?Saikolojia na Utafiti? ambacho kilizungumzia mbinu za kupona tatizo la nguvu za kiume baada ya kushirikiana na watafiti mbalimbali duniani. Ninachotaka uelewe ni kwamba tatizo hili linatibika, cha msingi ni kujua nini cha kufanya, sio kukata tamaa kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakifanya.

Msingi wa kuwa na maisha yenye amani ni kusaka tiba ya kile kinachokusumbua, sio kulia tu.

Tatizo huanzaje?; Umbile la mume lina sehemu (chambers) mbili muhimu ziitwazo corpora cavernosa, na corpora cavernosa.

Aidha kuna sehemu nyingine inaitwa The spongy tissue ambayo inajumuisha misuli na mishipa ya damu. Mwanzo wa tatizo hilo huanzia kwenye ubongo na kitendo cha mwanaume kushindwa kuwa imara ni dalili ya magonjwa mabaya hasa ya moyo, figo nk.

Hisia zinazoingia kwenye ubongo huamsha misuli inayopeleka hisia hizo kwenye umbo la mume. Ndio kusema kwamba kutosisimka ipasavyo kwa mume ni dalili kwamba mfumo wa damu hausukumi vizuri.

Kinachofanyika ni kwamba baada ya msisimko, damu hujaa kwenye eneo liitwalo corpora cavernosa, hapo ndipo mwanaume husisimka na kuwa mwenye nguvu.

Wenye magonjwa kama vile kisukari, figo, wenye kuendelea vileo, kutokula vizuri, kuvuta sigara, kuacha kufanya mazoezi na kujichua wana uwezekano wa asilimia 70 kupata tatizo la nguvu za kijinsia. Takribani asilimia 35 na 50 ya wanaume wenye ugonjwa kisukari, wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume.

Wengine walio katika hatari ya kupata tatizo hili ni wale wenye uzito wa kupita kiasi. Wengine kati ya asilimia 10 na 20 wanasumbuliwa na tatizo hili kwa sababu ya matatizo ya kisaikolojia, kwa mfano kama mwenzi wako alikufanyia jambo baya nk.

Tatizo hili kama nilivyoeleza ni kubwa, hadi ilifikia hatua Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama, 10 Aprili 2007 katika kikao cha saba cha bunge aliuliza swali ambalo lilikuwa namba 8 lenye kipengele a, b, na c ambapo kwenye kipengele b aliuliza: Je, serikali inafahamu ni sababu gani zinasababisha kupungua kwa nguvu za kiume kunakotangazwa sana na waganga wa jadi?

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Homeli Mwakyusa alijibu kuwa, upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi, baadhi yao ni lishe duni hasa mboga za majani, kutokula aina mbalimbali za jamii ya karanga (nuts), matumizi yasiyofaa ya ulevi kama pombe.

Alisema sababu nyingine kuwa ni matumizi ya sigara na dawa za kulevya, dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya akili na vilevile kutopumzika kunakosababishwa na shughuli nyingi za kijamii hivyo kusababisha uchovu.

Lakini ni kweli dawa hizi za asili zinauwezo wa kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Pro. Mwakyusa anathibitisha kwa kusema kuwa, dawa nyingi za tiba asili ni virutubisho ambavyo muhitaji angeweza kuvipata endapo angekula vyakula vyenye virutubisho hivyo. Pia haijawahi kuripotiwa mtu kuathirika baada ya kutumia dawa hizi.

Ninachotaka kusisitiza katika makala haya ni kwamba ikiwa una tatizo la nguvu za kijinsia, jambo la msingi ni kuangalia staili za maisha unayoishi hasa kwa kuachana na tabia zinazosababisha mtu kupata tatizo hili kama vile ulevi, kuacha kujichua, kujifunza namna ya kuishi na watu tofauti wakiwemo wale wanaokera nk.

Zaidi ya yote unapaswa kujua aina ya vyakula ambavyo ukila vinaweza kukuondolea tatizo hilo. Kwa kawaida kuna vyakula vya aina tofauti, kwa mfamo vya wagonjwa, watoto, watu wa ndoa nk.

Zaidi ya vitu vingine unavyopaswa kuvitumia, unatakiwa kwanza mwenye kutoa tiba kujua udogo au ukubwa wa tatizo. Kumbuka chakula ni chakula, lakini chakula ni tiba, ukitaka kuamini hili, kama una mafua chukua kitunguu swaumu, kiponde jipake chini ya unyayo utapona. Ndio nasema kwamba katika maisha tafuta mbinu za kuondokana na shida inayokukabili kwa njia ya amani, sio kujiua, atafute hufanikiwa, wala usichoke kuhangaika hadi upate unachotaka. 

Pia wengi wetu tumekuwa na imani kuwa kufanya kazi nyingi kupita kiasi kunatupa uwezo wa kushinda vishawishi vya ngono, hiyo ni sawa kabisa lakini ufahamu kuwa ipo siku utahitaji saikolojia yako itambue uwepo wa mwanamke / mwanaume ambaye ni mpenzi wako na anakuhitaji kimapenzi, hapo sasa ndio tatizo linakuja, uume haujazoea kuhusu maswala ya mapenzi. 

Jitahidi pale unapoweza kufanya akili yako ichangamke unapokuwa na mke/ mume wako na kusahau mambo ya kazi kwa muda muafaka, ili kufanikisha hilo fanya yafuatayo unapokuwa faragha na mwenzi wako;

(a) Hakikisha mnafunga mlango wa chumba mnachokitumia kwa ufunguo
(b) Hakikisheni wote wawili SIMU zenu za mkononi zipo off au silent ( zimezimwa inapobidi)
(c) Usalama wa chumba chenu ni wa uhakika, yaani watoto wasumbufu wasiwe karibu ili kuwavurugia muda muafaka, na ikibidi watoto kama wapo likizo wapeleke kwa bibi yao.

Huyo uliye naye ni mke au mume wako, kwa nini unamuonea aibu? Jjitahidi  sana kumpa uhuru wa kutosha kukuburudisha kuliko kuwa na haraka, unakimbilia wapi jamanii? mi ni wako tu honey wangu, mwendo wa kinyonga ndo unafaa katika kusisimua mishipa ya damu.

Wabongo tujitahidi kwenda vacation mara chache katika mwaka, hii inaleta ladha tofauti katika mapenzi kuliko kila siku kuwa na penzi katika kitanda kimoja tu, epuka sana kulala na mtoto mdogo kitanda kimoja wakati wa majambozi hiyo ni mbaya sana kisaikolojia, mwache mtoto alale na dada kwa dakika chache wakati nyie mnapeana raha kwa muda mlioupanga kisha mkamchukue na kuja kulala nae pale inapobidi.

Natamani kuongelea sana eneo hilo apo juu, lakini wabongo wengi hampendi kusikia ukweli kuhusu faragha bado hatujawa wazi kutenga muda wa faragha na hatimaye tuna ngonoka tu hata kama mtoto amelala kitanda tunachokitumia, tukiamini kuwa ni mtoto hajuwi kitu.

Kwa leo tuishie hapo, ukitaka kufahamu madhara ya kungonoka wakati mwanao kalala hapo pembeni usikose makala ya, MTOTO ALIYE KUZWA NA TABIA YA NGONO KUTOKA KWA WAZAZI WAKE sehemu ya 1.


UTAJITAMBUAJE KAMA UMESHIKA UJAUZITO? HIZI NI BAADHI TU YA DALILI ZITAKAZO KUFUNGUA KATIKA KUFAHAMU KAMA NI MJAMZITO AU LA!



DALILI KUMI NA TATU ZA MAMA MJAMZITO.
MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.
“Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadha ndani ya  mwili ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi kujua kama una ujauzito au la. Dalili hizo ni kama zifuatazo;
Maumivu kwenye matiti
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.
Maumivu mwilini
Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.
Kutokwa damu bila kutegemea
“Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai Inasemekana  kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.
Kuchoka
Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.
“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi.
Chuchu kuwa nyeusi
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, inasemekana: “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuziona dalili hzi mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”
Kichefuchefu
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
Mwili kuvimba
Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea, na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito, na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.
Kwenda haja ndogo mara kwa mara
Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.
Tamaa ya vitu mbalimbali
Kutokana na mwili kuwa na ‘mzigo’ wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka, kwa mfano, aina fulani ya vyakula, au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.
Kuumwa kichwa
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususan katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.
Kufunga choo
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo, hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unaendelea kukua.
Kuwa na hasira
“Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,
Kuongezeka kwa joto mwilini.
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna ‘mtoto anakuja’.