Wanawake Mashujaa Tanzania ni taasisi inayojitegemea, ikishirikiana na wadau mbalimbali pamoja na wafadhili katika kuyafikia malengo yake. Na siyo taasisi ya KIDINI, wala KISERIKALI, wala kibiashara na hivyo kuipa asilimia mia moja katika kuangalia mambo yote yanayoilenga Jamii hasa Mwanamke na Mwanaume. Hivyo unapotoa msaada utapelekwa moja kwa moja kwa muhusika bila kukwepeshwa au kutumiwa vibaya. Wanawake Mashujaa Tanzania tunakaribisha wadau na wafadhili waweze kuwasiliana nasi moja kwa moja bila kupitia kwa matapeli.
Wanawake Mashujaa Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuangalia mahusiano ya Mwanaume na Mwanamke kuanzia umri wa miaka 18 - 35 na kubahatika kugundua matatizo kadha wa kadha katika mahusiano hayo upande wa MAPENZI.
Wanawake Mashujaa Tanzania itakusaidia katika kupata ufumbuzi wa baadhi ya mataatizo hayo kisaikolojia na kukuwezesha kuendelea mbele bila kujutia maumivu ya nyuma, pia unapokuja kuonana nasi utapata muelekeo wa jinsi ya kutatua matatizo yanayokukabili katika mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi kifupi.
Unapokuwa na sisi utapata nafasi ya kuzungumza na washauri wetu kwa bei nafuu na kila mnachozungumza ni SIRI na kupeana faraja kisaikolojia ambayo ni tiba ya nafsi na akili.
Lengo kuu la Wanawake Mashujaa Tanzania ni kuhakikisha kila Mwanamke na Mwanaume walioamua kuanzisha mahusiano ya kimapenzi wanakuwa na furaha na amani tangu mwanzo wa mahusiano hadi mwisho wa mahusiano na kuamua kuingia katika taasisi ya NDOA na kuishi kama mume na mke kihalali.
Kwa habari ya Watoto na malezi tupo kumsaidia Mwanaume na Mwanamke ambao wanahitaji kupanga Uzazi salama na kuwa na familia bora. Tupo kwa ajili yako kukupa ushauri juu ya njia za uzazi wa mpango salama.
Pia tunatoa huduma ya Ushauri nasaha na kupima, tunawaandaa kisaikolojia na kisha tunawaelekeza katika kliniki ya karibu itakayowasaidia kupata huduma ya kupimwa afya na kufahamu kama hamjaambukizwa virusi vya ukimwi.
Wanawake Mashujaa Tanzania ni wajibu wetu kuangalia watoto yatima siku za sikukuu na kuwatia moyo kwa kucheza nao, kuwapa zawadi, kula nao chakula n.k pia tunahuduma mbalimbali za kutembelea wanawake mahosipitali na magerezani ili kuwapa moyo na kuwasaidia kisaikolojia ili waweze kujikubali na kuendelea mbele.
Kwa ufupi naamini utakuwa umepata picha ya kile tunachokifanya kama Wanawake Mashujaa Tanzania ni zaidi ya hayo na mazuri sana kwa ajili yako. KARIBU SANA NA ALIKA WENGINE TUJADILI PAMOJA.
No comments:
Post a Comment