Friday, August 3, 2012

FAHAMU SAIKOLOJIA YA JINSIA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI KWA UNDANI, ITAKUSAIDIA KUJITAMBUA NA KUMTAMBUA MWENZI WAKO KIURAHISI!

MWANAUME NI NANI KATIKA JAMII?

o        Mwanaume ni kiongozi wa familia
o        Mwanaume ni mlinzi wa mwanamke pamoja na familia
o        Mwanaume ni mfano wa kuigwa na jamii
o        Mwanaume ni mrithi wa Mungu

MWANAUME MWENYE ASILI YA MUNGU (MWENYE MAADILI MAZURI)

o   Ni mnyenyekevu wakati wote
o   Ni mvumilivu wakati wote
o   Yupo tayari kusuluhisha kesi yake na kuanza upya
o   Ni mwepesi kusamehe na kusahau
o   Ni mtu mwenye utu na anathamini utu wa mtu
o   Anajali watoto na mke wake pia
o   Hatakama atakuwa si muaminifu hujitahidi sana mke wake asijue

MWANAUME MWENYE ASILI YA DUNIA (ASIYE NA MAADILI MAZURI)

o   Ni mkorofi kupindukia
o   Hana utu wala kujali
o   Ni mtu wa lawama wakati wote
o   Hana hofu kwa chochote anachokifanya
o   Huhesabu makosa wakati wote
o   Hana maneno ya faraja kila wakati hulaani tu
o   Hana moyo wa kusamehe, siyo rahisi kesi yake imalizike kwa amani

v  Kundi la kwanza linamtambulisha mwanaume mwenye anayefuata muongozo mzuri wa malezi kutoka kwa wazazi wake na pia sheria za dini ambazo zinamuandaa kuwa mwanaume mwenye majukumu ya mke na familia. Hivyo anapokutana na mwanamke asiye na maadili inamuwia vigumu sana kumbadilisha tabia na kama Mungu asipoingilia kati mahusiano haya kunaweza kumfanya mwanaume huyu asitamani tena kuoa au kuwa katika mahusiano maana huwaza kupenda na endapo atapata mwanamke mwenye maadili ndoa yao itakuwa nzuri sana kutokana na asili yao.

v  Kundi la pili linamtambulisha mwanaume asiye na malezi na asiye jua nini wajibu wake kama mwanaume. Mwanaume huyu anakuwa katika hali kama hii endapo kwa upande mmoja wazazi wake walichangia katika malezi mabovu au wazazi walijitahidi sana kumfundisha lakini hakufundishika, Mwanaume huyu anapokutana na mwanamke mwenye maadili au aliyefundishwa vizuri tangu mwanzo kuwa ipo siku moja atakuwa mke wa mtu itamuwia vigumu mke huyu kuchukuliana na huyu mwanaume na atahangaika sana kutaka kumbalisha lakini haitawezekana kwa kipindi kifupi tu. Itamlazimu kulipa gharama ya muda mrefu na kumtafuta Mungu zaidi kuliko kutumia akili zake mwenyewe.

v  Katika makundi yote haya tunaweza kuona mwanaume uliyenae wewe yupo katika kundi gani na asili gani ili unapoanza kushugulika na kasoro unazoziona katika ndoa au mahusiano yako utambue mwanaume huyo asili yake ni nini na jinsi gani utaweza kusaidiana naye katika safari hii ya mahusiano au ndoa yenu.


MWANAMKE NI NANI KATIKA JAMII?

o   Mwanamke ni msaidizi wa mwanaume
o   Mwanamke ni taji ya mwanaume
o   Mwanamke ni mjenzi wa mji wake na nyumba yake
o   Mwanamke ni kipenzi cha watoto na mume
o   Mwanamke ni mwalimu wa familia
o   Mwanamke ni mshawishi wa tabia njema kwa jamii inayomzunguka

MWANAMKE MWENYE ASILI YA MUNGU (MWANAMKE MWENYE MAADILI)

o Hana haraka ya mambo
o Mvumilivu, mnyenyekevu, mtiifu, mkweli, anaheshima, anajituma, ana utu
o Yupo tayari kufanya suluhu na kusahau
o Yupo tayari kujifunza kutokana na makosa
o Ana mapenzi ya dhati nay a ukweli
o Anajali watoto na mume wake pia pamoja na jamii yote inayomzunguka
o Hayupo tayari kumsaliti mume wake hata kama sababu zote anazo.

MWANAMKE MWENYE ASILI YA DUNIA (ASIYE NA MAADILI)

o  Ni mkorofi
o  Hasira zake huwa karibu na za wazi wazi sana
o  Kinywa chake hutoa matusi na lawama wakati wote
o  Hukusanya makosa ya mume wake wakati wote
o  Huwa na upendo wa mtego, hana upendo wa dhati
o  Hupenda kupokea zaidi ya kutoa
o  Hulazimisha mambo yafanyike hata kama haiwezekani kwa wakati huo.

v   Katika kundi la kwanza tunamuona mwanamke mwenye asili ya mungu ambaye hutambulika kama mwanamke shujaa mwenye maadili ya kuwa mke mwema na aliye andaliwa vizuri kuwa mke bora kwa mume na familia nzima, Mwanamke huyu anapokutana na mwanaume mwenye asili ya dunia hujuta sana kwanini ameingia katika mahusiano na mtu huyu, inamuwia vigumu kuikabili tabia ya mwanaume huyu na kuona wanaume wote ni maadui na kama ikishindikana kupata msaada wa kumtoa katika eneo hilo basi hujikuta akibaki mnyonge na mwenye kilio wakati wote hatimae kutokuwa katika mahusiano tena. Anapobahatika kukutana na mwanaume ambaye ana maadili mahusiano yao huwa ya amani sana na hata ndoa yao huwa inadumu kwa kiasi kikubwa sana.

v  Kundi la pili linamtambulisha mwanamke asiye na malezi na asiye jua nini wajibu wake kama mwanamke. Mwanamke huyu anakuwa katika hali kama hii endapo kwa upande mmoja wazazi wake walichangia katika malezi mabovu au wazazi walijitahidi sana kumfundisha lakini hakufundishika, Mwanamke huyu anapokutana na mwanaume mwenye maadili au aliyefundishwa vizuri tangu mwanzo kuwa ipo siku moja atakuwa mume wa mtu itamuwia vigumu mume huyu kuchukuliana na huyu mwanamke na atahangaika sana kutaka kumbalisha lakini haitawezekana kwa kipindi kifupi tu. Itamlazimu kulipa gharama ya muda mrefu na kumtafuta Mungu zaidi kuliko kutumia akili zake mwenyewe.

v  Katika makundi yote haya tunaweza kuona mwanaume uliyenae wewe yupo katika kundi gani na asili gani ili unapoanza kushugulika na kasoro unazoziona katika ndoa au mahusiano yako utambue mwanaume huyo asili yake ni nini na jinsi gani utaweza kusaidiana naye katika safari hii ya mahusiano au ndoa yenu.

MAPENZI NI NINI?

Kutokana na tafsiri mbali mbali na mijadala mbali mbali inaonesha mapenzi ni ‘’ mkusanyiko wa hisia za binadamu zinazopelekea kujenga urafiki wa kudumu kati ya mwanamke na mwanaume au mtu na mtu mwingine.’’

MPENZI NI NANI?

o   Ni binadamu aliyejitoa kwa ajili yako, kusaidiana na wewe katika shida na raha
o   Ni mtu yeyote aliyetayari kuumizwa kwa ajili yako
o   Ni binadamu aliye tayari kushauriana na wewe pale anapoona umekosea
o   Ni binadamu aliyetayari kuona unafanikiwa badala ya kuangauka
o   Ni binadamu aliyetayari kushirikisha hisia zake za kimapenzi na wewe bila kificho

KUFANYA MAPENZI NI NINI?

o   Kuonesha hisia zako za kimapenzi kwa vitendo
o   Kufanya vitendo vya upendo kwa wale wote walio shirikiana na wewe ktika shida au raha
o   Kujitoa kwa jamii nzima zaidi ya kusubiri kupokea zaidi

KUSUDI LA KUFANYA MAPENZI NI NINI?

o   Kumfurahisha mpenzi wako
o   Kufurahisha mwili wako na nafsi yako
o   Kupata watoto/ kuanzisha familia kwa kupata watoto
o   Kujenga ushirikiano wa kudumu baina yako na mwenzi wako/ jamii inayokuzunguka
o   Kuonesha hisia za mapenzi kwa vitendo na kufanya suluhu ya matatizo yenu.

MAPENZI YANABEBWA NA VITU VIWILI VIKUBWA AMBAVYO NI:
UPENDO NA HISIA ZA MAPENZI.

UPENDO NI NINI?

v  Ni tendo la hiari kutoka moyoni mwa mtu analo kusudia kulifanya kupitia vitendo vya ukarimu, upendo siyo kujivuna, siyo kujisikia wewe ni bora kuliko wengine, siyo kulipiza kisasi, siyo kulaani bali kubariki n.k

v  Upendo ni kusaidiana katika raha na shida pia kutoa shukurani kwa Mungu na jamii nzima pale unapokuwa umeshirikiana nao katika jambo lako lolote.

v  Upendo husaidia kumaliza ugomvi na kufanya jamii nzima iwe na amani

v  Upendo mara nyingi unapokuwa ni wa dhati hauwezi kupotea kamwe kwani kila sku vitendo vya upendo husaidia kuongeza ladha ya mahusiano. Hivyo unapoona vitendo vya upendo vinapungua katika nyumba yako ujue ni rahisi kupoteza amani iliyomo humo ndani.

v  JUKUMU LAKO KAMA MWANAUME AU MWANAMKE ULIYE KATIKA MAHUSIANO NI KUPENDA KWA DHATI ILI KUFANYA VITENDO VYA UPENDO VIZAE AMANI KATIKA NYUMBA YENU NA MAHUSIANO YENU.

HISIA ZA MAPENZI NI NINI?

o   Hapa kila mmoja wetu atakuwa na jibu lake kuhusu swali hili lakini hebu na tuziangalie hisia za penzi ni nini maana yake.

o   Hisia za mapenzi ni ile hali isyo kifani, msisimko, shauku, kujiskia raha mara zote unapoona mwenzi wako anarudi kutoka katika shughuli za kila siku, au anarudi kutoka safari, au anapokuwa karibu na wewe.

o   Hisia za mapenzi ni tendo linalonesha mapenzi ya dhati kati ya wewe na mpenzi wako jinsi mlivyoshibana.

o   Hisia za mapenzi ni nzuri kupindukia ndo maana mamilioni ya wasanii wa muziki duniani kote wamekuwa wakiimba nyimbo zinazolenga mapenzi na wapenzi.

o   Wengi wetu tumeshapatwa na hisia za mapenzi kali sana kiasi kwamba tumebaki tukijilaumu na kufikia hatua ya kujiua au kuwaua wale wanaoingilia mapenzi yetu. Hisia za mapenzi zaweza kujenga undugu wa kudumu na waliokaribu yako au kubomoa/kuvunja undugu na waliokaribu yako.

UKWELI KUHUSU HISIA ZA MAPENZI UPOJE?
o   Hisia za mapenzi hujengwa na vitendo vya upendo
o   Hisia za mapenzi huweza kutoweka na kuhamia mahali popote pale penye upenyo ambapo vitendo vya upendo hupatikana kwa urahisi.
o   Hisia za mapenzi huweza kurudisha mapenzi yaliyoharibiwa vibaya kwa kupata vitendo vya upendo wa dhati mara dufu ya ilivyokuwa mwanzo.
v  Tatizo ulilonalo leo katika NDOA yako au mahusiano yako ni vyema ukalifanyia uchunguzi mapema ili kujuwa kama limetokana na kushuka kwa kiwango cha UPENDO hivyo kupelekea HISIA ZA MAPENZI kupotea na kuvunja amani yako na mpenzi wako.

·         FANYA TATHIMINI YA MAHUSIANO YAKO, NA UJIHOJI MASWALI YAFUATAYO!
(i)                 Unauhakika kuwa unafahamu hisia za mapenzi, na unajuwa zinachochewa na vitedo vya upendo?
(ii)               Unafahamu gharama ya kupoteza vitendo vya upendo?
(iii)             Upo tayari kupoteza NDOA/MAHUSIANO kutokana na kutokuwa mtafiti wa mbinu mbali mbali za kudumisha mahusiano au ndoa yako?
(iv)             Ulishawahi kumpenda mume / mke wako kwa vitendo?
(v)               Unatarajia nini kutoka kwa mume/ mke wako unapofanya vitendo vya upendo?  (b) Unatarajia kupokea zaidi au kutoa zaidi?
(vi)             Wewe ni muaminifu kwa kila jambo katika mahusiano uliyopo? (b)  Unauwezo gani wa kusimamia uaminifu wako na mwenzi wako linapokuja tatizo la KUKOSA UAMINIFU?
(vii)           Upo tayari kusamehe na kusahau? (b) Je upo tayari kucheza vizuri katika nafasi yako?
(viii)         Upo tayari kupanga mambo yako upya? (b) Upo tayari kuangalia mazuri ya mwenzako na kukumbuka mazuri aliyokutendea kuliko kuangalia mabaya na makosa madogo madogo anayokosea eidha kwa kujuwa au kutokujuwa kama kwako ni makosa?

MAMBO YA KUANGALIA NA KUZINGATIA KATIKA SWALA LA MAPENZI!
(i)                 Kumbuka kuwa penzi ni kitendo, kitendo cha kumjali na kumfikiria mwenzi wako na kuwa mpole, muungwana, mwenye subira, na kuelewa kuwa huyo mpenzi wako ana uhuru wa kuweza kuchagua kukupenda au kutokukupenda milele bila kuangalia hasara zitakazopatikana.
(ii)               Kumbuka kuwa hisia za penzi ni hisia tu, zinaweza kuja kwa wingi au zinaweza kutoweka kabisa.
(iii)             Endapo utaona hisia za penzi zimeanza kutoweka unaweza kufanya jitihada kuzirudisha kwa kufanya matendo ya upendo bila kujali faida au hasara zitakazotokea, unachohitaji hapa ni kurudisha penzi lako katika mstari ulionyooka!
v  Ili kudumisha NDOA yenu au mahusiano yenu itakutegemea wewe kama wewe eidha ni mwanamke / mwanaume. Kwa upande wa mwanamke ana paswa kuonesha upendo zaidi kuliko kupokea, isipokuwa pale ambapo mwanaume ameshindwa kabisa kupokea upendo wako na


Imeandaliwa na Diana D. Shirima
Muanzilishi - Wanawake Mashujaa Tanzania

2 comments:

 1. MARA NYINGI MWANZILISHI WA UPENDO/NDOA NI MWANAUME KWANI NDIYE ANAYEMTAFUTA MWENZA, LAKINI KWA SABABU WANAWAKE WENGI (SIO WOTE)WANAWEZA KUFICHA UHALISI WAO NA KUVAA UHALISIA WAA MUDA WANAHARIBU MAHUSIANO/NDOA KWANI WAZUNGU HUSEMA "FACT IS FACT ALWAYS" NASEMA HIVYO KWA SABABU NA MIMI YAMENIKUTA JAPO SIJAWAHIMKUONA MWANAMKE MKOROFI NA MWENYE KIBURI KM HUYU. HAPENDI NDUGU, MAAMUZI YA MUME HAYAHESHIMU, MARAFIKI WA MUMUE HATA KAMA NI WABAYA BASI, HAWAPENDI. ANATAKA ANACHOKITAKA YEYE. AKISEMA PIGA UPIGE WAKATI HUO HUO, FUKUZA UFUKUZE WAKATI HUOHUO, FANYA LOLOTE UFANYE WAKATI HUOHUO, UKISUBIRI ILI UTAFAKARI HATAKI NA MARA NYINGI ANASUSA. KWA UJUMLA MAISHA MAZURI YANATEGEMEA MWANAMKE AWE NA BUSARA KTK MAMBO YOTE, NA HATA BIBLIA INASEMA "MWANAMKE MPUMBAVU HUIVUNJA NYUMBA YAKE MWENYEWE NA MWANAMKE MWENYE BUSARA HUIJENGA NYUMBA YAKE MWENYEWE"KWA NINI ASIAMBIWE MWANAUME? MUNGU ALIJUA WANAWAKE WANA UDHAIFU KTK MAHUSIANO HATA AKAMWAMBIA MWANAUME KUWA MTAISHI NA WAKE ZENU KWA AKILI. SISEMI HIVYO KWA KUWA MIMI NI MWANAUME LA! LAKINI NDIVYO MAMBO YALIVYO.WATU WENGI TUNAWALAUMU WANAUME KWA KUWA WANAWAPIGA/WAUA WAKE ZAO BILA KUJIULIZA KWA NINI WANAFANYA HIVYO, WANAFANYA HIVYO KWA SABABU WAO NDIO WALIKUWA WA KWANZA KUMPENDA MWANAMKE WAKIDHANI BAADA YA HAYO YALE ALIYOKO AKILINI (MAENDELEO)YATAANZA KUPATIKANA BADALA YAKE YANATOWEKA MOJA BAADA YA JINGINE. KUSEMA UKWELI WANAUUME KABLA HATUJAOA TUNAKUWA NA MIPANGO MINGI YA KUENDELEZA FAMILIA TOFAUTI NA WANAWAKE. MAENDELEO YA NYUMBANI HAYAPANGWI NA MWANAMKE BALI YANASIMAMIWA NAE.WANAUME WANA MIPANGO MINGI YA MAENDELEO LIKIWEPO LA KUWATUNZA HATA WAZEE NA KUENDELEZA MIJI YAO. KINACHOSHANGAZA BAADA YA KUOA, MWANAMKE HUANZA KUPANGUA MOJA BAADA YA JINGINE NA HAPO NDIPO AONEKANAPO KUWA NI MKOROFI. KUENDELEZA UPANDE WA KIKENI SIO JAMBO LA KULAZIMISHWA KWA WANAUME KWANI MARA NYINGI WANAWAKE HUPENDA MAENDELEO YAANZE KWAO BILA KUJUA/WAKIJUA KAKA ZAO WAKIFANYA HIVYO KWA MAWIFI ZAO WAO NDIO WA KWANZA KULUMBANA NA MAWIFI. KIMSINGI PAULO KTK BIBILIA ALILIONA HILI KUWA NI SHIDA NA AKASHAURI NI HERI KILA MTU AKAE MWENYEWE LAKINI KWA KUWA MIILI YETU HUTAMANIANA BASI KILA MMOJA NA AWE NA MWENZI. NAJUA KILA UPANDE UTAVUTIA KWAKE LAKINI KM ULIVYOAINISHA MAJUKUMU, MWANAUME NI KICHWA JAPO SIO WOTE NA UDHAIFU WA MMOJA USICHUKULIWE KM WOTE NDIVYO WALIVYO (KUWAONA WAMAUME/WANAWAKE WOTE NDIVYO WALIVYO)

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ndugu yangu nimekupata vizuri sana, lakini tunachotamani ni kuona kila mmoja anajitambua na kutaka kukabiliana na changamoto anazozikuta katika mahusiano ya kimapenzi, wakati mwingine tunakuwa wagumu kuelewa na kukabiliana na yale yanayotusibu, sasa unahisi tukiachana na kukimbilia kwa wapenzi wapya ndo kuna usalama? Hebu fikiria kama kila mmoja wetu akiwa na mawazo hasi kuhusu ndoa yake, na kuamua kuishi kivyake ni nani atabaki katika ndoa? Kwa kweli hakuna atakayebaki ndio maana mashirika ya dini, taasisi mbali mbali zinazungumza sana kuhusu ndoa, mahusiano na n.k kwani wote wameona taabu iliyo mbele, sasa tatizo limepata dawa lakini NANI ANAKUBALI KUNYWA HIYO DAWA? TUNALIA NA KUFUNGA KWA MAOMBI TUKIOMBA WENZI WETU WABADILIKE LAKINI ASILI ZETU NA UTU WETU WA KALE HATUJAUACHA, SASA UNAOMBEA NINI? UKIRUDI NYUMBANI UNAMTUKANA MWENZIO? HUO SI UNAFIKI?

   NI LAZIMA TUKUBALI KUBADILIKA NA KISHA TUSAHAU MADHAIFU YETU, SIO KILA SIKU TUNAKUMBUSHIANA TU MAKOSA, NA HII NI KWA MWANAMKE NA MWANAUME.

   Delete