Wednesday, November 28, 2012

SEHEMU YA PILI YA MADA KUHUSU NDOA, NA MAISHA YA NDOA!

Natumai hujambo kabisa mpendwa wangu unaefuatilia makala zangu za NDOA, NDOA, UILILIAYO UNAWEZA KUITUMIKIA?  Ni swali ambalo limekuwa likiwaumiza watu wengi walio katika mahusiano na wengi zaidi ambao wanatamani kuingia katika mahusiano, leo tuangalie baadhi ya vitu ambavyo wengi wetu tumekuwa tukihisi tutavikuta katika mahusiano ya kimapenzi na endapo tukivikosa basi mahusiano huwa katika usawa wa kuvunjika au kuwa na migogoro isiyo kwisha.

UBINAFSI

 Huu nimeutafsiri kama kigezo cha kila aliepo katika mahusiano ya kimapenzi kuwa nacho kwa kusudi eidha zuri au baya, nasema hivi kwa sababu wote wawili tunavoingia au kutamani kuingia katika mahusiano huwa tunalenga kupokea vitendo vya mapenzi zaidi kutoka upande wa pili (mpenzi) huuangalii kama na wewe unahusika asilimia zile zile uoneshe kumpenda mwenzako, sasa kasheshe linakuja pale ambapo mwenzio anahitaji kujipendelea zaidi yeye apendwe, ni kwanini unataka upendwe wewe zaidi? Huyo akupendaye atapendwa na nani? wakati mwingine tumekuwa tukilaumu zaidi upande mmoja bila kugundua huo ni UBINAFSI, unakusumbua, jiachie alafu fanya zaidi ya vile unavyotamani ufanyiwe na mpenzi wako kisha utaona mabadiliko au siyo? Acha kulalamika na tafuta suluhu kwa amani!

TAMAA

Tamaa imechukua nafasi kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi kwani kila mmoja anatamani kutendewa vizuri sana na mpenzi wake katika mambo mengi sana, hivyo basi unapokuwa nje ya mahusiano ya kimapenzi huwa unatamani kufanya mambo mengi mazuri kwa mwenzio na mpenzi wako anakuwa anajiandaa kupokea zaidi kutoka kwako, gafla unapoingia katika mahusiano kila kitu kinabadilika kiasi kwamba hadi zile ahadi na mapenzi uliyoahidiwa hayaonekani, unadhani nini kitafuata? Kila mmoja huonesha ubabe wake halisi na kujitoa taratibu katika uhusiano bila upande mmoja kuelewa kinachoendelea. Umeshafahamu ni kwa nini mpenzi wako ana tabia aliyonayo sasa hivi? Angalia muenendo mzima wa tabia zake jinsi alivyobadilika kisha chukuwa hatua ya kujirekebisha wewe kwanza alafu ndo mkae pamoja kurekebishana!

Natamani kuendelea, lakini mda hauniruhusu kwa sasa, tuendelee kuwa pamoja wakati mwingine!
Ndo kwanza kumekucha, usichoke kusoma makala haya na upende kubadilika rafiki yangu na ujitahidi kusaidia wengine wabadilike.

Nakupenda na natamani ubadilike ili tuibadilishe jamiii yetu!

Imeandaliwa na,
Diana D. Shirima
Founder - Wanawake Mashujaa Tanzania

No comments:

Post a Comment