MAISHA KWA UJUMLA BAADA YA KUJIFUNGUA!
Baada
ya kujifungua pamoja na kuwepo na mabadiliko mbalimbali maisha yanaendelea kama
kawaida huku mapenzi zaidi yakielekezwa kwa mtoto. Mama asianze kazi ngumungumu
hadi amalize miezi mitatu.
Tendo la ndoa linaweza kuanza muda wowote baada ya kujifungua ili mradi mama hana tatizo lolote kiafya ingawa uangalifu mkubwa unahitajika ili asipate ujauzito haraka haraka.
Tendo la ndoa linaweza kuanza muda wowote baada ya kujifungua ili mradi mama hana tatizo lolote kiafya ingawa uangalifu mkubwa unahitajika ili asipate ujauzito haraka haraka.
Unyonyeshaji ukazaniwe kwani husaidia kizazi kurudi katika hali ya kawaida,
damu kukata haraka, mtoto kuwa na afya na pia ni njia ya uzazi wa mpango.
Mama anaweza kuanza kutumia njia ya uzazi wa mpango wa vidonge majuma matatu
tangu atoke kujifungua kama hanyonyeshi kwa sababu zozote zile au kama
ananyonyesha anaweza kuanza kutumia vidonge hivyo miezi mitatu toka ajifungue.
Mama pia anaweza kuanza mazoezi ya kupunguza tumbo baada ya majuma sita, na
pia katika kipindi hiki anaweza kufunga tumbo.
Usibweteke ndugu yangu pamoja na furaha ya kupata mtoto usisahau kuwa baba nae anakuhitaji na amemiss ukaribu wako kwa muda mrefu sana!
No comments:
Post a Comment