Monday, October 29, 2012

TIBA KWA WANAUME IMEKUJA, SOMA HAPA UPATE ELIMU JUU YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UPATE MSAADA WA KISAIKOLOJIA.



 Tatizo la wanaume wengi la kukosa nguvu za kiume sasa limepata ufumbuzi wa hali ya juu kutoka kwa watafiti mbalimbali ambao hawalali mchana na usiku wakihangaika kupata ufumbuzi huu, na hizi ndio habari mpya walizonazo kwako wewe unaesumbuliwa na tatizo hili, karibu sana upate somo hapa!

Tafiti mbalimbali duniani zinabainisha kunaongezeko kubwa la watu wanaosumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume,  (ED au Erectile dysfunction).

Kulingana na taarifa za shirika liitwalo the National Ambulatory Medical Care Survey (NAMCS), nchini Marekani kati ya wanaume 1,000, watu 22 husumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume/kijinsia hasa wale wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea juu.

Aidha kutokana na kukithiri kwa tatizo hilo, NAMCS inasema zaidi ya watu 2.6 milioni wanatumia dawa za kuongeza nguvu za kiume. Hali ni mbaya pia nchini, hii ndio sababu kuna matangazo mengi ya waganga wa jadi wenye kutibu nguvu za kijinsia, kiasi kwamba inakuwa vigumu kufahamu yupi mkweli yupi mwongo.

Utafiti pia unaonyesha kuwa asilimia 5 ya wanaume wenye umri wa 31- 40 na kuendelea wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo, aidha kati ya asilimia 15 na 25 na wanaume wenye umri wa miaka 65 wanakabiliwa na tatizo hili.

Nimewahi kupitia  vitabu kadhaa, kwa mfano kile kiitwacho ?Saikolojia na Utafiti? ambacho kilizungumzia mbinu za kupona tatizo la nguvu za kiume baada ya kushirikiana na watafiti mbalimbali duniani. Ninachotaka uelewe ni kwamba tatizo hili linatibika, cha msingi ni kujua nini cha kufanya, sio kukata tamaa kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakifanya.

Msingi wa kuwa na maisha yenye amani ni kusaka tiba ya kile kinachokusumbua, sio kulia tu.

Tatizo huanzaje?; Umbile la mume lina sehemu (chambers) mbili muhimu ziitwazo corpora cavernosa, na corpora cavernosa.

Aidha kuna sehemu nyingine inaitwa The spongy tissue ambayo inajumuisha misuli na mishipa ya damu. Mwanzo wa tatizo hilo huanzia kwenye ubongo na kitendo cha mwanaume kushindwa kuwa imara ni dalili ya magonjwa mabaya hasa ya moyo, figo nk.

Hisia zinazoingia kwenye ubongo huamsha misuli inayopeleka hisia hizo kwenye umbo la mume. Ndio kusema kwamba kutosisimka ipasavyo kwa mume ni dalili kwamba mfumo wa damu hausukumi vizuri.

Kinachofanyika ni kwamba baada ya msisimko, damu hujaa kwenye eneo liitwalo corpora cavernosa, hapo ndipo mwanaume husisimka na kuwa mwenye nguvu.

Wenye magonjwa kama vile kisukari, figo, wenye kuendelea vileo, kutokula vizuri, kuvuta sigara, kuacha kufanya mazoezi na kujichua wana uwezekano wa asilimia 70 kupata tatizo la nguvu za kijinsia. Takribani asilimia 35 na 50 ya wanaume wenye ugonjwa kisukari, wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume.

Wengine walio katika hatari ya kupata tatizo hili ni wale wenye uzito wa kupita kiasi. Wengine kati ya asilimia 10 na 20 wanasumbuliwa na tatizo hili kwa sababu ya matatizo ya kisaikolojia, kwa mfano kama mwenzi wako alikufanyia jambo baya nk.

Tatizo hili kama nilivyoeleza ni kubwa, hadi ilifikia hatua Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama, 10 Aprili 2007 katika kikao cha saba cha bunge aliuliza swali ambalo lilikuwa namba 8 lenye kipengele a, b, na c ambapo kwenye kipengele b aliuliza: Je, serikali inafahamu ni sababu gani zinasababisha kupungua kwa nguvu za kiume kunakotangazwa sana na waganga wa jadi?

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Homeli Mwakyusa alijibu kuwa, upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi, baadhi yao ni lishe duni hasa mboga za majani, kutokula aina mbalimbali za jamii ya karanga (nuts), matumizi yasiyofaa ya ulevi kama pombe.

Alisema sababu nyingine kuwa ni matumizi ya sigara na dawa za kulevya, dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya akili na vilevile kutopumzika kunakosababishwa na shughuli nyingi za kijamii hivyo kusababisha uchovu.

Lakini ni kweli dawa hizi za asili zinauwezo wa kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Pro. Mwakyusa anathibitisha kwa kusema kuwa, dawa nyingi za tiba asili ni virutubisho ambavyo muhitaji angeweza kuvipata endapo angekula vyakula vyenye virutubisho hivyo. Pia haijawahi kuripotiwa mtu kuathirika baada ya kutumia dawa hizi.

Ninachotaka kusisitiza katika makala haya ni kwamba ikiwa una tatizo la nguvu za kijinsia, jambo la msingi ni kuangalia staili za maisha unayoishi hasa kwa kuachana na tabia zinazosababisha mtu kupata tatizo hili kama vile ulevi, kuacha kujichua, kujifunza namna ya kuishi na watu tofauti wakiwemo wale wanaokera nk.

Zaidi ya yote unapaswa kujua aina ya vyakula ambavyo ukila vinaweza kukuondolea tatizo hilo. Kwa kawaida kuna vyakula vya aina tofauti, kwa mfamo vya wagonjwa, watoto, watu wa ndoa nk.

Zaidi ya vitu vingine unavyopaswa kuvitumia, unatakiwa kwanza mwenye kutoa tiba kujua udogo au ukubwa wa tatizo. Kumbuka chakula ni chakula, lakini chakula ni tiba, ukitaka kuamini hili, kama una mafua chukua kitunguu swaumu, kiponde jipake chini ya unyayo utapona. Ndio nasema kwamba katika maisha tafuta mbinu za kuondokana na shida inayokukabili kwa njia ya amani, sio kujiua, atafute hufanikiwa, wala usichoke kuhangaika hadi upate unachotaka. 

Pia wengi wetu tumekuwa na imani kuwa kufanya kazi nyingi kupita kiasi kunatupa uwezo wa kushinda vishawishi vya ngono, hiyo ni sawa kabisa lakini ufahamu kuwa ipo siku utahitaji saikolojia yako itambue uwepo wa mwanamke / mwanaume ambaye ni mpenzi wako na anakuhitaji kimapenzi, hapo sasa ndio tatizo linakuja, uume haujazoea kuhusu maswala ya mapenzi. 

Jitahidi pale unapoweza kufanya akili yako ichangamke unapokuwa na mke/ mume wako na kusahau mambo ya kazi kwa muda muafaka, ili kufanikisha hilo fanya yafuatayo unapokuwa faragha na mwenzi wako;

(a) Hakikisha mnafunga mlango wa chumba mnachokitumia kwa ufunguo
(b) Hakikisheni wote wawili SIMU zenu za mkononi zipo off au silent ( zimezimwa inapobidi)
(c) Usalama wa chumba chenu ni wa uhakika, yaani watoto wasumbufu wasiwe karibu ili kuwavurugia muda muafaka, na ikibidi watoto kama wapo likizo wapeleke kwa bibi yao.

Huyo uliye naye ni mke au mume wako, kwa nini unamuonea aibu? Jjitahidi  sana kumpa uhuru wa kutosha kukuburudisha kuliko kuwa na haraka, unakimbilia wapi jamanii? mi ni wako tu honey wangu, mwendo wa kinyonga ndo unafaa katika kusisimua mishipa ya damu.

Wabongo tujitahidi kwenda vacation mara chache katika mwaka, hii inaleta ladha tofauti katika mapenzi kuliko kila siku kuwa na penzi katika kitanda kimoja tu, epuka sana kulala na mtoto mdogo kitanda kimoja wakati wa majambozi hiyo ni mbaya sana kisaikolojia, mwache mtoto alale na dada kwa dakika chache wakati nyie mnapeana raha kwa muda mlioupanga kisha mkamchukue na kuja kulala nae pale inapobidi.

Natamani kuongelea sana eneo hilo apo juu, lakini wabongo wengi hampendi kusikia ukweli kuhusu faragha bado hatujawa wazi kutenga muda wa faragha na hatimaye tuna ngonoka tu hata kama mtoto amelala kitanda tunachokitumia, tukiamini kuwa ni mtoto hajuwi kitu.

Kwa leo tuishie hapo, ukitaka kufahamu madhara ya kungonoka wakati mwanao kalala hapo pembeni usikose makala ya, MTOTO ALIYE KUZWA NA TABIA YA NGONO KUTOKA KWA WAZAZI WAKE sehemu ya 1.


No comments:

Post a Comment