Sunday, November 25, 2012

NDOA, NDOA, NDOA, UNAYOILILIA JE UPO TAYARI KUITUMIKIA?





Habari ya leo mpendwa wangu, napenda kusaidiana na wewe katika mada yetu ya leo kama inavyojieleza katika kichwa cha habari hapo juu.

Mimi na wadau wenzangu wa maswala ya familia na maadili tumekuwa tukijiuliza maswali mengi kuhusu NDOA na MAISHA YA NDANI YA NDOA, na kung'amua yafuatayo ambayo kwa upande mmoja au mwingine yanaweza kukusaidia katika maamuzi ya kujiandaa kuingia katika taasisi hii kabla hujavamia au kujikuta unajuta baada ya muda mfupi sana.

Ni muda mrefu sana tumeshuhudia wanawake wengi sana wakifunga kwa maombi na wengine wakienda kwa waganga wa jadi kusafisha nyota ili waweze kupata waume wa kuwaoa/ na wanaume pia wamekuwa wakisumbuliwa sana na hali hii hatimaye nawao wanahangaika kutafuta wakuweza kuoa na kuishi nae milele. Siyo mbaya kabisa kufikia uamuzi/ maamuzi hayo, lakini swali ni kwamba Je? umejiandaa vipi kuishi maisha ya ndani na huyo unaemtaka? au unayemuombea kila siku? Muda mwingi wengi wetu tumekuwa tukitamani kitu ambacho kwa nje huwa hatukielewi haraka, badala yake tumekuwa tukiamua kirahisi rahisi tu ili kutimiza ndoto zetu za kuwa mume/mke wa mtu bila kuangalia ni jinsi gani tunaenda kuishi huko ndani, wengine huwa mnasema, " haina shida, nkifika ndani, nitajitahidi kumrekebisha, na hiyo tabia ya ulevi kupindukia ataiacha." unahisi ni kazi rahisi kumbadilisha mtu mzima ambaye ukoo wake mzima ni yeye tu ndo anakunywa bia laini, na walio salia wote wanywaji wa GRANTS na WISKY? unahisi wazazi wake walivokuwa wanamsisitiza apunguze ulevi walikuwa wajinga? Leo wewe ambaye hujajipanga chochote zaidi ya kelele zako na mdomo wako mchafu, ndo utambadilisha? Hebu jiulize swali hili, wazazi na ndugu zake tangu anakuwa walizoea kumuona akija nyumbani saa sita usiku, huwa hawasemi kitu, wewe leo na sheria zako mpya unamfokea tu na kumlazimisha arudi saa mbili, inawezekana kweli kirahisi?

Mwingine yeye hayawahi kuona baba na mama yake wakikaa mezani kula pamoja hata siku moja, sana sana wageni wakija ndo wanaweza kukaa pamoja tena wale wageni wa muhimu sana, leo wewe umetoka katika familia yenu, kila siku jioni ni lazima wote muwe mezani (dinning) kwa chakula, na huwa mna mazoea ya kusali kabla ya kula na pia mkimaliza kula mnasali kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya siku hiyo kisha kila mmoja anatawanyika kwenda kulala, sasa mume wako au mkeo hana tabia hiyo na kwake ni kero kubwa pale unapomlazimisha, unafanyaje kukabiliana na swala hilo? Kila unapojitahidi kumuhamasisha aje mezani yeye haoni umuhimu, amekazana kuangalia TV, au kakazana kuchat na friends zake wa facebook and tweeter, inakuwaje? Duuuu! kama nakuona vile unavyonuna usiku mzima, unajijutia lakini ufanyaje? tayari ushaingia kwenye ndoa ndugu yangu!

Ni mambo mengi sana yapo katika hii mada, ila kwa leo tunaishia hapo natamani sana kuendelea ila mda hautoshi na mie sitaki usome kama gazeti kwani kujifunza ni kidogo kidogo, na umuhimu ni kufunguka ulipojifunga au siyo ndugu yangu? Usijali tupo pamoja na tutafika tu au siyo jamaniiii?

Hadi wakati mwingine, usikose kufuatilia makala nyingine inayoendeleza habari zaidi kuhusu NDOA, NA MAISHA NDANI YA NDOA!

No comments:

Post a Comment