Monday, December 3, 2012

SEHEMU YA TATU NA YA MWISHO KWA MWAKA 2012, MADA ILIYO PANA NA INAYOSHIKILIA MAISHA YA WAPENDANAO ILIKUWA, NDOA,NDOA UNAYOILILIA UNAWEZA KUITUMIKIA?



Ndugu zangu wapendwa, napenda sana kutumia wakati huu kumshukuru Mungu aliyeniwezesha katika safari nzima ya mwaka 2012 nikiwa kama mwanaharakati mchanga katika gurudumu hili la Familia, Malezi na Mapenzi.

Ki ukweli hakuna kazi rahisi hapa duniani, kila jambo unalolifanya linachangamoto zake na mara zote nimejifunza kuvumilia na kusimama katika maono niliyonayo hadi kieleweke.

Unaweza ukasema kuwa wanaharakati wengi wanajiingiza katika uharakati kwa manufaa yao wenyewe, lakini mimi kama mimi ninapenda kusema kwamba uanaharakati nilianza tangu nikiwa mtoto mdogo, nakumbuka nikiwa darasa la pili Jijini Arusha, ndoto yangu ilikuwa niwe mama bora kwa familia yangu, mke mwema, na mwanamke shujaa kwa jamii inayonizunguka, namshukuru sana Mungu kwa asilimia 98%  nimefanikiwa kufikia malengo yangu.

Mara nyingine nimekutana na vikwazo mbalimbali hasa katika hatua za ukuaji, kama kijana wa kike nilipitia mengi sana, mengine kwa kujua na mengine kwa kutokujua lakini yote ya yote niliyaita mapito hayo kama DARASA kwangu ili leo niwe msaidizi wa kuwafungua wengine wanaopita katika maeneo niliyopita kwa ujasiri.

Unajua maana ya UJASIRI?  Ngoja leo nikudokeze japo kidogo, ujasiri maana yake ni kuvuka katika eneo gumu na kuendelea kuwa na uso wenye tabasamu la kudumu huku ukinyooshewa vidole na jamii husika. Unapojifunza kujikubali, ukatubu, ukabadilika na kusonga mbele tayari wewe ni SHUJAA. Ndio maana leo hii mimi nimesahau yote niliyoyatenda katika ujana wangu, nikajitambua na sasa nipo vizuri kusaidia jamii inayonizunguka iweze kutambua wajibu wao katika maisha ya kila siku.

Katika kai hii namshukuru Mungu nimekamilisha mwaka mmoja tangu niianze rasmi, niliianza kama kujitolea, baadae nikatoa fomu za kujiunga na chama ambazo bado zipo na zinauzwa kwa Tsh: 5,000/=  natumai kutokana na gharama za uendeshaji kuwa mgumu kila mwanachama mpya wa 2013 atakayependa kujiunga na chama atapaswa kuchangia Tsh. 10,000/=  ili tuweze kufikia malengo ya chama chetu ifikapo mwaka 2015.

Naamini jamii ya Tanzania inakilio kikubwa sana kuhusiana na swala hili la mahusiano, ndoa na maisha ndani ya ndoa. Lakini mbona wahusika tumekaa kimya? mbona kila kitu kipo wazi na tunaona jinsi ambavyo hali imekuwa mbaya katika maisha ya mahusiano alafu hatustuki, tunaona sawa tu! Hebu angalia waliopo nyuma yako, angalia kizazi kinachokuja hapo nyuma kutakuwa na NDOA kweli?

Sasa ndugu zangu naomba tusijisahau katika hili, tunahitaji mchango wenu ili kufikia malengo ya kuwasaidia wote waliopo katika mahusiano na walioingia katika taasisi ya ndoa ili wajitambue na kukaa katika mstari ulionyooka. Wewe na mimi tunaweza kuibadilisha mitazamo hasi kuwa chanya kuhusu mahusiano mema katika mapenzi na maisha ndani ya ndoa.

Naamini kabisa malengo yangu yatatimia katika swala hili la uanaharakati wa maswala ya familia, malezi na mahusiano ya kimapenzi, ili ifikapo 2015 tuwe tumeifikia Tanzania nzima kwa kutoa mafundisho na kusaidiana kuhusu saikolojia ya mapenzi na malezi ya watoto.

Nna mengi ya kuzungumza, lakini naomba nisikuchoshe, endapo utapenda kuwasiliana na mimi kwa ajili ya kujiunga na chama hiki, kufadhili chochote basi usisite kuwasiliana na mimi kwa namba zifuatazo:

DIANA DIDAS SHIRIMA
FOUNDER - WANAWAKE MASHUJAA TANZANIA
+255 766 44 57 33 / 682 622 626
didasdiana@gmail.com
www.wanawakemashujaatanzania.blogspot.com

MUNGU WA MBINGU NA NCHI AKUBARIKI SANA KWA KUJITOA KWA AJILI YA JAMII, MKE, MUME, NA WATOTO WAKO AMBAO WANAKUZUNGUKA! 
PAMOJA TUNAWEZA, KUBWA NI KUJIAMINI TU!

No comments:

Post a Comment